Posts
MAN U YAZIDI KUPAA KUIFUKUZIA TOP 4
- Get link
- X
- Other Apps
Jana jumapili ligi kuu ya EPL iliendelea kutimua vumbi katika viwanja viwili tofauti. Huku mchezo wa mapema kabisa ukipigwa katika dimba la Sundeland ambapo wenyeji walikuwa wakijaribu kutupa karata yao dhidi ya mabingwa wa kihostoria Manchester United ili angalau kujaribu kujinasua mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo walimokuwamo mpaka sasa Lakina bahati haikuwa yao kwani mpaka dk 90 za mchezo zinamalizika Sunderland 0 3 Man Utd, huku mabao ya Man Utd yakifungwa na Ibrahimovic, Mikhitaryan na Rashford katika dakika za 30, 46 na 89, Mchezo mwingine hiyo jana ulikuwa kati ya Everton ambao bado wanapambana vizuri dhidi ya mabingwa watetezi ambao kama wameamka toka usingizini baada ya kushinda mechi mfululizo, lakii Everton waliwaonyesha kazi baadaa ya kuibuka washindi kwa jumla ya Goli 4-2, Lukaku peke yake akitupia wavuni goli na hivyo kuzidi kung'ang'ania kileleni katika orodha ya wafungaji bora Epl akiwa amefikisha magoli 23 akifuatiwa na Hanry Kane wa Spurz...